Mkuu wa Mkoa amebainisha kuwa, Serikali ngazi ya Mkoa itaendelea kupokea taarifa kutoka Wizara ya Afya kuhusiana na ugonjwa wa kipindupindu ili kuhakikisha Jamii inapata taarifa kamili kuhusiana na ugojwa huo ambao tayari umeshaanza kulipuka nchi za jirani.
“Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini , Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kutoa taarifa na takwimu za kuwepo mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu kuanzia mwezi Septemba 2023 katika baadhi ya nchi jirani kama vile Msumbiji na Zambia pamoja na baadhi ya Mikoa nchini” alisema Mkuu wa Mkoa.
Sambamba na hilo Mhe. Batilda Burian ameweka wazi mmoja ya mkakati utakaotumika katika kupambana na ugojwa huu ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na ugonjwa huu wa Kipindupindu, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha elimu inawafikia wananchi wote.
“Hatuna budi kuwaelimisha Wananchi na kuchukua tahadhari mapema ya kujikinga na ugonjwa huu hatari unaoambukiza kwa haraka sana kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia kula chakula au kunywa maji na vinywaji vingine kama juisi n.k. vilivyochafuliwa na vimelea vya Kipindupindu” aliongeza Mhe. Batilda Burin.
Mbali na kutoa elimu kwa Umma, Mkoa tayari umeshaandaa mpango maalumu wa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huu kwa kuwahusisha watalaamu wa Afya ambao watakuwa mstari wa mbele katika kupambana na mlipuko wa ugonjwa huu.
Ameleeza kuwa “Tumeandaa mpango mkakati wa Mkoa (Regional Cholera outbreak Contigency plan) wa kukabiliana na Mlipuko wa Kipindupindu endapo utatokea katika Mkoa wetu. Mpango umeianisha maeneo ya kujengea uwezo kwa wakati huu wa kujiandaa kukabiliana na ugonjwa huu na hatua za kuchukua endapo ugonjwa utaingia mkoani kwetu.”
Aidha Mhe. Mkuu wa Mkoa ameendelea kumshukuru Mhe. Dkt. Sambia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha ambazo zimehimarisha kikamilifu miundombinu ya afya ambayo kwa hakika imerahisha utoaji wa huduma ya Afya na hasa sasa kwenye uwekaji wa mipango ya kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.
“Kwa kipekee natoa shukrani za dhati kwa Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mapinduzi makubwa aliyoyafanya kwenye Sekta ya Afya kwa kipindi cha miaka miwili na nusu ya uongozi wake” alisema Mhe. Mkuu wa Mkoa.
Mpaka sasa Mkuu wa Mkoa ameagiza Uongozi wa Halmashauri uvifahamishe vituo vyote vya kutolea huduma za Afya kuchukua tahadhari na kutoa Elimu ya Afya kwa wagonjwa na ndugu wa wagonjwa kujikinga na ugonjwa huu , Halmashauri zote ziandae vituo maalum tengefu (cholera Treatment Centre) watakapohudumia wagonjwa wenye Kipindupindu ,Halmashauri ziandae Mpango kazi wa kupambana na kudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu kwa kushirikisha sekta muhimu za Afya, Maji na Elimu, na Maafisa Afya kusimamia na kufanya ukaguzi wa huduma na biashara za chakula, wahakikishe zinatolewa kwa kufuata kanuni na sheria za Afya
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa