Na. Robert Magaka – Tabora.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Tabora, Bi. Asha Churu, leo asubuhi amewasilisha zawadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan,kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Tabora katika vituo mbalimbali vya huduma za jamii. Zawadi hiyo imetolewa katika vituo vya kulelea watoto yatima, wazee na walemavu, ikiwemo Nyumba ya Huruma ya Mama Teresa, Chuo cha Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu RwanzaIi, na Kituo cha Kulelea Watoto Waliotelekezwa cha Nyumba ya Matumaini Cheyo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Bi. Churu amemshukuru Mhe. Rais kwa msaada huo muhimu ambao utasaidia vituo hivyo kuyamudu maisha ya kila siku. Vitu vilivyotolewa ni pamoja na mafuta ya kula, mbuzi, mchele, unga wa ngano, mahindi, na juisi – bidhaa zitakazosaidia katika kuboresha hali ya kimaisha ya wanufaika.
Wanufaika wa msaada huo, wakiwemo wazee, watoto na walemavu, walijumuika kwa furaha kutoa shukrani zao kwa Mhe. Rais Samia. Wamemshukuru kwa msaada huo wa kipekee na kumtakia heri, afya njema, na mafanikio katika uongozi wake.
Misaada hii ni sehemu ya juhudi za serikali ya Rais Samia katika kusaidia makundi yaliyo katika mazingira magumu na kuhakikisha kuwa wanapata huduma muhimu kwa ustawi wa jamii.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa