Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko ametembelea na kukagua mradi wa umeme kutoka Tabora hadi Urambo na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme kilichopo Wilayani Urambo
Mradi huo unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 132 mpaka kukamilika kwake Juni 30, 2024 unatarajia kugharimu jumla ya shilingi Bilioni 40 ikiwa ni fedha kutoka serikali kuu (Fedha za ndani).
Kukamilika kwa mradi huu kutaboresha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika Wilaya ya Urambo, Kaliua na mkoa wa Tabora kwa ujumla na kuchoche shughuli za uzalishaji kwa wananchi na kukuza pato la taifa.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa