KITUO CHA OPERESHENI CHA DHARURA ZA AFYA YA JAMII KUFUNGULIWA MKOANI TABORA
Wizara ya afya kwa kushirikiana na shirika la afya Dunian (WHO) wanaendesha mafunzo kwa wasimamazi wa afya ngazi ya mkoa .
Mafunzo hayo yanafanyika katika Mji wa Nzega kwenye ukumbi wa Titete .
Daktari wa mkoa wa Tabora Dkt .Honoratha Rutatinisibwa akifungua mafunzo hayo jana Tarehe 18 Novemba,2024 amesema anaishukru wizara ya Afya pamoja na shirika la afya Dunian kwa kuamua kituo Cha operasheni cha dharura ya Afya ya jamii kufunguliwa Tabora .
na amewaasa wanamafunzo kuhakikisha wanasikiliza kwa umakini wanayo fundishwa ili yakalete tija kwenye kituo hicho alisema."
Kwa upande wake mkuu wa msafara wanafunzo hayo kutoka wizara ya afya Dkt.Agnes Buchwa amesema tupo hapa kuhakikisha washiriki wanapata kile kinacho stahili na kwamba tutatumia mbinu zote ili washiriki waweze kuelewa hata mitihani tutatoa ili tuone wapi hawaja elewa tutie mkazo zaidi alisema Dkt.Agnes
Mafunzo hayo yatajumuisha kwa nadhalia na vitendo yatakuwa ya muda wa siku tano ambapo yamenza Jana tarehe 18 Novemba mpaka tarehe 22 Novemba yatakapo hitimishwa rasmi.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa