Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Paul Matiko Chacha amekuwa miongoni mwa wakuu wa mikoa 13 walioshiriki kwenye mkutano wa mwaka wa wadau wa Tumbaku kitaifa uliofanyika leo Machi 28, 2024 jijini Dodoma.
Mkutano huo ulifunguliwa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe wenye malengo ya kuangalia maendeleo ya zao la tumbaku na tafiti mbalimbali zinazohusiana na zao hilo.
Tumbaku ni zao linalolimwa mkoani Tabora na mikoa mingine 12 ambapo zaidi ya asilimia 95 ya zao hilo huuzwa kwenye masoko ya nje ya nchi ambapo mauzo yake yameongezeka kutoka Dola za Marekani 106,278,461!47 mwaka 2020/2021 hadi kufikia Dola za Marekani 389,556,750 mwaka 2023/2024 kufikia Desemba 2023 na bado mauzo yanaendelea.
Aidha, Mkutano umeshirikisha wadau wengi wakiwemo Wakuu wa Mikoa inayozalisha Tumbaku; Wabunge kutoka Majimbo yanayozalisha Tumbaku; wanunuzi; wasindikaji; wachakataji; watafiti; Agriculture Council of Tanzania; Taasisi za Fedha; Vyama Vikuu vya Wakulima wa Tumbaku; na Wasambazaji wa Pembejeo.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa